Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Wilaya ya Amirul-Mu’minin Ali (as) ina maana ya kuwa na uhusiano usiovunjika naye katika fikra na matendo. Amirul-Mu’minin (as) katika Nahjul-Balagha ameielezea Qur’ani kuwa ni mwongozaji na mshauri mwaminifu asiyeghushi, mtu ambaye haioni Qur’ani kuwa inaweza kueleweka au ambaye hayuko tayari kujitolea mali na nafsi yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hana Wilaya ya namna hiyo, Wilaya ni kuingia katika ngome ya Mwenyezi Mungu na kupata usalama dhidi ya adhabu Yake.
Mfululizo maalumu wa “Tusome Qur’ani” unaelezea tafsiri za Qur’ani kutoka kwa Kiongozi Shahidi, katika sehemu hii, tutachunguza mada ya “Jamii ya Kiislamu humsogeza mwanadamu karibu na Mwenyezi Mungu”, na hapa chini tunawasilisha matini yake kwa wasomi kama ifuatavyo:
Wilaya ya Ali bin Abi Talib ina maana gani?
Ina maana kwamba katika fikra zako uwe mfuasi wa Ali;
Katika matendo yako uwe mfuasi wa Ali;
Uwe umefungwa na Ali bin Abi Talib (as) kwa uhusiano wenye nguvu, imara na usiovunjika;
Usijitenge na Ali;
Hiyo ndiyo maana ya Wilaya. Je, mmeelewa vizuri maana ya Wilaya ni nini?
Hapa ndipo tunapoelewa maana ya Hadithi hii:
«وَلاَیةُ بن اَبیطالِبٍ حِصنِی»
“Wilaya ya Ali bin Abi Talib ni ngome yangu” — kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu —
«فَمن دَخَلَ حِصنی اَمِنَ مِن عَذاِبی»
“Yeyote atakayeingia katika ngome yangu atakuwa salama na mwenye amani dhidi ya adhabu Yangu.”
Haya ni maneno ya kuvutia sana.
Yanamaanisha nini?
Yanamaanisha kwamba; Waislamu wafuasi wa Qur’ani, ikiwa kwa upande wa fikra na mawazo yao, na pia kwa upande wa matendo, juhudi na harakati zao, watakuwa wameunganishwa na Ali bin Abi Talib, basi watakuwa salama na wamelindwa dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Je, si hivyo?
Je, kuna maana nyingine isipokuwa hiyo?
Iwapo Ali bin Abi Talib atafahamika leo, na baada ya kufahamika sisi na nyinyi tutende kama alivyotenda, hapo ndipo tutakapopata Wilaya.
Wilaya ina maana hiyo.
Mimi ambaye naiona Qur’ani kuwa haiwezi kueleweka — bila shaka mimi naielewa, Mungu aepushe mbali nisije nikasema Qur’ani haiwezi kueleweka; ninamkusudia yule mtu ambaye haioni Qur’ani kuwa inaweza kueleweka — mtu huyo anawezaje kusema kuwa ana Wilaya ya Ali bin Abi Talib na kwamba kwa upande wa fikra ameunganishwa na Ali, ilhali Ali bin Abi Talib katika khutba ya Nahjul-Balagha anasema:
«وَ اعلَموا اَنَّ هذَا القُرآنَ هُوَ النّاصِحُ الذی لا یغش والهادی الذی لایضل وَالمُحَدِّثُ الُّذی لایکذب وما جالس هذا القرآن احد الا قام عَنهُ بِزِیادَةٍ اَو نقصانٍ زِیادَةٍ فی هُدًی اَو نقصانٍ مِن عَمًی»
“Jueni kwamba Qur’ani hii ni mshauri ambaye haghushi, ni mwongozaji ambaye hapotezi, na ni msemaji ambaye hadanganyi. Hakuna yeyote anayekaa pamoja na Qur’ani hii isipokuwa huondoka nayo akiwa ama ameongezeka katika uongofu au amepungua katika upofu.”
Amirul-Mu’minin (as) kwa namna hii anawarejesha watu kwenye Qur’ani, kwa namna hii anawasukuma watu kuielekea Qur’ani.
Yule mtu anayesema kwamba Qur’ani haiwezi kueleweka, je, ana Wilaya ya Ali bin Abi Talib?
Kamwe, hapana.
Ali bin Abi Talib kwa ajili ya Mwenyezi Mungu yuko tayari kujitoa kikamilifu; hayo matendo ya Ali.
Lakini mtu huyu hayuko tayari kutoa hata kiasi kidogo cha mali yake, wala nafsi yake, wala hadhi yake ya kijamii, wala starehe yake, wala ukuu wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Je, huyu ana Wilaya ya Ali bin Abi Talib?
Wilaya ya Ali bin Abi Talib anayo yule ambaye ameunganishwa na Ali kwa kiungo kisichokatika;
Kwa upande wa fikra na mawazo,
Na pia kwa upande wa matendo.
Chanzo: Kitabu Tarh-e Kulli-ye Andishe-ye Islami dar Qur’an (Muhtasari wa Mfumo wa Fikra ya Kiislamu Katika Qur’ani), mlango wa Wilaya, kikao cha 24, uk. 431.
Maoni yako